Skip to content
Maabara ya Akiolojia ya Pleistocene (PAL)

Maabara ya Akiolojia ya Pleistocene (PAL) ni kituo kipya cha utafiti katika Taasisi ya Historia- CSIC (Baraza la Kitaifa la Utafiti la Uhispania), lililoko Centro de Ciencias Humanas y Sociales, CCHS, Madrid. Maabara hii inalenga kukuza utafiti juu ya akiolojia ya mageuzi ya binadamu, zana za kale za mawe na utafiti wa jamii za wawindaji katika kipindi cha Pleistocene.

PAL inajuhusisha na tafiti za kiakiolojia hasa tafiti juu ya asili ya teknolojia. Utafiti huu unajumuisha uchimbaji wa kiakiolojia nchini Afrika ya Mashariki na Uhispania, tafiti za zana za mawe zinazofanyika PAL zinahusisha utafiti wa teknolojia ya mawe, majaribio ya kunakili na alama za matumizi.

Utafiti na kazi ya maabara

PAL imeundwa kwa dhumuni la kukuza utafiti unaohusisha vipengele mbalimbali vya mabadiliko ya Mageuzi/mabadiliko ya binadamu katika akiolojia ya Pleistocene, ikiangazia zaidi uchunguzi wa zana za mawe. Hii inajumuisha uchunguzi wa technologia/taipolojia, majribio ya kurudufu na uchunguzi wa matumizi.

Hizi sasa, PAL inahifadhi mikusanyo kutoka maeno mablimbali ya tafiti ya zana za mawe duniani. Pia, inahifadhi mikusanyo ya kipekee ya majaribio itokanayo na mtumizi ya mawe asilia kama vile Chert, Lava na Quartzite kutoka Ulaya na Afrika.

Pamoja na shughuli za kawaida za kitafiti zinazohusu zana za mawe na akiologia ya mageuzi ya binadamu, PAL pia inatoa fursa kwa makampuni ya kibiashara ya kiakiologia, ikijumuisha tathmini ya athari na uchimbuaji wa tabaka la Pleistocene, uchambuzi na uchapishaji wa mikusanyo ya zana za kale.

Maabara yetu ina nyenzo wezesha za kufanyia hatua zote za kichunguzi zinazohusu zana za mawe kama vile, miundombinu maalumu ya kuhifadhi taarifa, skena ya 3D, mashine za kuchapisha QR codes, vifaa vya kupiga picha, hadubini za kawaida na za 3D, vifaa maalumu na vya kisasa vya utafiti wa uwandani kama vile Total station, hadubini bebeka na nyenzo muhimu za uchimbuzi wa zana za kale za mawe.

Mafunzo kwa Vitendo

Tunawakaribisha wanafunzi wanaotaka kupata uzoefu kwa vitendo katika akiolojia ya zana za mawe kupitia mpango wa Erasmus+.

Lengo kuu la mafunzo haya ya vitendo ni kukutambulisha kuhusu miradi inayoendeshwa na PAL. Mafunzo yatahusisha pamoja na mengineyo, kuielewa taswira nzima ya mikusanyo ya kiakiologia inayohifadhiwa na PAL. Kama kituo bora cha utafiti wa vitendo, PAL inakupa fursa ya kufanya kazi na mikusanyo ya zana za kale za mawe zenye uhusiano kimataifa na kupata uzoefu kwa vitendo katika mikusanyo ya kiakiologia.

Huduma za ushauri elekezi zitolewazo na PAL

  • Chunguzi za kiakiologia na uchimbaji
  • Uzalishaji wa mifano ya 3D ya za zana za kiakiolojia
  • Kuweka ramani za maeneo ya kiakiolojia
  • Utafiti wa alama za matumizi na teknolojia katika mifupa na mawe.
  • Ushauri elekezi juu ya akiolojia na jioakiolojia ya Pleistocene, na jamii ya wawindaji.
  • Michoro elekezi ya kiakiolojia
  • Shughuli za uhamasishaji
  • Utafiti wa zana za mawe za jamii za wawindaji
  • Utafiti wa majaribio wa mfuatano wa upunguzaji wa zana za mawe kabla ya historia

Kwa habari zaidi tafadhali wasiliana nasi