Skip to content

EF-HR

EF-HR liko katika upande wa Kaskazini mwa Bonde la Olduvai, wastani wa kilomita 1.3 magharibi kutoka Ufa wa Tatu. Liligunduliwa mnamo mwaka 1931 na Sir Evelyn Fuchs na Profesa Hans Reck, na likapewa jina la waanzilishi hao. Uchimbaji wa kwanza ulifanywa na M. Leakey mnamo mwaka 1963, na kisha OGAP walirudia tena uchimbaji kwenye eneo hilo mnamo mwaka 2009.

EF-HR ni mojawapo ya maeneo ya awali ya zana za Acheulean huko Olduvai, ingawa stratigrafia iliyopendekezwa na OGAP inapendekeza kuwa EF-HR iko juu katika mfuatano wa tabaka la pili (Bed II) kuliko ilivyopendekezwa hapo awali, ambayo ina athari katika utambuzi wa umri halisi wa eneo hilo, ambao kwa sasa unakadiriwa kuwa karibu miaka milioni 1.5 iliyopita.

Picha za juu za maeneo ya utafiti ya EF-HR kama zilivyochukuliwa na ndege zisizo na rubani.

Maeneo ya utafiti ya EF-HR kwa upana.

Mfano wa miinuko ya DEM katika eneo la EF-HR kama ilivyochukuliwa na ndege isiyo na rubani.

OGAP imepanua eneo alilochimba Leakey kuelekea kaskazini, na kuchimba maeneo kumi na moja zaidi kwenye eneo la takribani kilomita moja za maraba, ili kuchukua sampuli katika vipindi sawa vya kistratigrafia kama ilivyo katika eneo kuu la uchimbaji katika mandhari hii pana ya kale. Uchimbaji wa kiakiolojia wa OGAP kwenye eneo kuu na maeneo yaliyo karibu umefukua mkusanyiko mpya mkubwa, wenye zaidi ya visukuku 3,000 na zana za kale, ikiwa ni pamoja na mamia ya shokamkono (Handaxe) katika nafasi zake za kistratigrafia.

Picha mchanganyiko za maeneo ya utafiti ya eneo kuu la EF-HR.

Mtazamo wetu wa uchimbaji wa kimajaribio katika maeneo tofauti umegundua tofauti dhahiri katika msongamano wa zana za kale katika maeneo yote, pamoja na kundi kubwa la nyenzo za kiakiolojia ndani na karibu na eneo kuu la uchimbaji, na kiwango kidogo cha shughuli za kibinadamu katika usawa mmoja kulingana na umbali pambazoni mwa maeneo ya uchimbaji.

Mpangilio wa maeneo ya utafiti katika eneo kuu la EF-HR.

Video fupi ya juu kwenye maeneo ya utafiti ya EF-HR, iliyochukuliwa na OGAP kwa kutumia ndege isiyo na rubani.

Trachyte-trachyandesite cleaver kutoka EF-HR eneo namba 2.

Eneo hili lilitafsiriwa na Mary Leakey kama kambi ya muda iliyoko kando ya mkondo mdogo wa maji. Walakini, hivi karibuni utafiti wa kiikolojia unaonyesha kuwa eneo kuu la EFHR lilikuwa kwenye sehemu ya kina kabisa laa bonde lililochimbwa kutokana na mmomonyoko wa mto, na matokeo yetu yanaonyesha kuwa hatua hii ilikuwa muhimu kwenye mkusanyo.

Mary Leakey aliichukulia teknolojia ya EF-HR kuwa tofauti na mikusanyo mingi katika eneo la kati na la juu katika tabaka la pili (Bed II), kutokana na idadi kubwa ya shokamkono (handaxes) zilizochongwa kutokana na majabali na mawe mviringo makubwa.

Uchimbaji katika eneo la EF-HR uliofanywa na OGAP.

Matokeo ya utafiti katika eneo namba 2 EF-HR zikitandazwa kimlalo.

Michoro waridi ya T2-Eneo kuu la uchimbaji katika makundi ya zana na katika maeneo yalikatwa kwa kina na mikondo ya maji.

Tazama pia maeneo ya Olduvai: MNK Skull na HWK EE