Skip to content

HWK EE

HWK EE (Henrietta Wilfrida Korongo Mashariki Mashariki) iko katika sehemu ya kusini-mashariki ya Eneo la Makutano huko Olduvai Gorge. Eneo la HWKEE lilichimbwa kwa mara ya kwanza miaka ya 1970 na Mary Leakey, na kisha na kufanyiwa utafiti na mradi wa Akiolojia wa Olduvai Gorge kati ya 2009 na 2015. Ni eneo la mabaki ya zana za Oldowanzilizotengenezwa karibu miaka milioni 1.7 iliyopita. HWK EE pia linasadikika kuwa mojawapo ya maeneo ya mwisho ambapo Homo habilis aliishi huko Olduvai Gorge, na hivyo ni muhimu kwenye kutafiti tabia na tamaduni zilizo pelekea kutokea kwa teknolojia ya Acheulean na zamadamu waitwao Homo erectus katika eneo hilo.

Muonekano wa 3D wa eneo la HWK EE.

Eneo la HWK EE lipo katikati ya mpaka wa tabaka la chini na la Kati ya kitanda cha kijiolojia cha II. Muda huu ni muhimu katika kuelewa mwanzo wa tamaduni/teknolojia ya Acheulean kwenye bonde la Olduvai. Uchimbaji wetu katika eneo la HWK EE umetoa mojawapo ya mkusanyo mkubwa zaidi ya visukuku na mabaki ya vifaa vya zamadamu ambayo yana uwiano wa matabaka ya kijiolojia, na yamesambaa na kulingana na maeneo mengine ya uchimbaji wa ki akiolojia katika bonde hilo.

Mwonekano wa angani wa machimbo ya HWK EE.

Muundo wa mwinuko wa kidijitali wa eneo la HWK EE.

Picha za karibu za eneo la HWK EE kutoka angani.

Matokeo ya utafiti yanaonyesha msongamano mkubwa wa visukuku na zana za mawe kwa marefu ya matabaka ya stratigrafia na katika mapana ya eneo la karibu 300 m 2 , yakiangazia muunganiko wa visababishi vya kibayolojia na sizivyo hai katika uundaji wa makusanyiko haya. Ukubwa na utofauti wa mkusanyiko, pamoja na uhifadhi wake mzuri, unathibitisha eneo la HWK EE kama tovuti cha marejeo ya utafiti wa tekinolijia ya Oldowan huko Olduvai Gorge na kwingineko barani Afrika.

Makadirio ya msongamano (a) Makadirio ya eneo lenye makusanyo ndani ya HWK EE (b), kulingana na uwingi wa makusanyo kwenye eneo.

Usambaaji toka chini kwenda juu wa visukuku na zana za mawe katika matabaka ya  kiakiolojia ya HWK EE.

Mkusanyiko mkubwa wa visukuku vya mamalia uliochimbuliwa kutoka eneo la HWK EE unaonyesha ushahidi wa makazi ya muda mrefu, ikimaanisha kuwa eneo hilo lilikua lina mazingira ya kuvutia kwa zamadamu. Kulikuwa na chanzo cha maji katika eneo hilo, kikithibitishwa na uwepo wa samaki. Pamoja na eneo kubwa kuwa tambarare, palikua na miti ya kivuli pia.

Maelezo ya muingiliano baina ya zamadamu na mamalia katika eneo la HWK EE, kulingana na ushahidi wa kiakiolojia. Picha na Benoit Clarys

Mfupa wa mguu wa tembo kutoka HWK EE wenye alama za kukatwa na zana za mawe, ikiashiria uwezo wa zamadamu wa kupata chakula kutoka kwenye mizoga ya tembo miaka milioni 1.7 iliyopita.

Mabaki ya alama za kwenye mifupa yanaonyesha kuwa zamadamu alikuwa anapata kiwango kikubwa cha nyama na mafuta ya ndani ya mifupa kutoka kwenye mizoga ya wanyama mbalimbali, ikiwemo wanyama wakubwa. Hata hivyo, ushahidi wa uwepo mkubwa wa wanyama wanaokula nyama unamaanisha zamadamu walikua wanapata nyama na mafuta hayo kwa kuvizia mabaki ya mizoga ilioachwa na wanayama wala-nyama.

Visukuku na zana za mawe kutoka kwenye shimo kuu la uchimbaji katika eneo la HWK EE.

Makusanyo ya zana za mawe kutoka HWK EE ni makubwa yakiwa na vipande zaidi ya 18,000. Matokeo ya tafiti zetu yanaonyesha kuwa utengenezaji wa zana ulikuwa wa haraka, unaotumia muda mfupi zaidi, usio na ufundi mdogo zaidi, na unaozalisha zana chache ukilinganisha na makusanyo mengine ya zana za Oldowan. Hata hivyo, haraka katika kutenegeza zana za mawe na idadi ndogo ya zana zinazotengenezwa ulizingatia chaguzi maalumu ya aina ya malighafi ya mawe ya kutumia, pamoja na kunoa zana zilizotengenezwa.

Jiwe la lava linalo bondwa ili kupata zana, kutoka eneo la HWK EE.

Zana za mawe za Quartzite kutoka eneo la HWK EE.

Uwepo wa zana za mawe zenye sifa tofauti katika eneo moja unatufanya tujiulize tena kuhusu imani iliokuwepo awali kuwa teknolojia ya Oldowan ilikuwa na zana za aina moja pekee. Pia, hili linaonyesha kuwa, hata kabla ya uwepo wa teknolojia ya juu ya Acheulian, bado mikakati na uelevu mkubwa ulikuwepo na kuhitajika ili kuweza kuunda zana za Oldowan.

Jiwe la lava linalo bondwa ili kupata zana, kutoka eneo la HWK EE.

Kipande cha zana za mawe kilicho nolewa makali kutoka eneo la HWK EE.

Tazama pia maeneo ya Olduvai: MNK Skull Site na EF-HR.