Skip to content

OLDUVAI GORGE

Olduvai Gorge, kaskazini mwa Tanzania, inatambulika kimataifa kwa ugunduzi maarufu wa Louis na Mary Leakey wa binadamu wa awali na zana za kale adhimu zinazozilizohifadhi historia ya mabadiliko ya matumizi ya zana za mawe za mababu zetu, wanyama, na mazingira katika kipindi cha miaka milioni mbili iliyopita.

Utafiti katika bonde la Olduvai ulianza takribani karne moja iliyopita, ukitoa utajiri wa kipekee wa taarifa za kiakiolojia na kianthropologia kwa ajili ya tafiti za baadhi ya hatua muhimu za mabadiliko ya awali ya binadamu.

Bonde la Olduvai lilikuwa mahali pa mwanzo ambapo alama za awali za matumizi ya zana za mawe zilitambuliwa, na kupewa jina Oldowan, katika kipindi cha miaka milioni 2.6 na milioni 1.5 kilichopita. Olduvai pia ni eneo la awali katika Afrika ambapo zana za mawe za awali za Acheulean ziligunduliwa na mtazamo wa kimapokeo wa mageuzi ya Oldowan-Acheulean ulianzishwa.

Olduvai Gorge (Tanzania)

Kutoweka kwa tamaduni za awali zaidi za wanadamu, Oldowan, na nafasi yake kuchukuliwa na teknolojia mpya, Acheulean, ni moja ya mada kuu katika Paleoanthropolojia ya kisasa. Mradi wa Akiolojia wa Olduvai Gorge (OGAP) unaleta pamoja timu ya kimataifa ya wanaakiolojia, wanaikolojia na wanajiolojia, ambao lengo kuu ni kuchunguza taratibu zilizosababisha asili ya Acheulean katika Olduvai Gorge.

OGAP ni nini?

Ili kuchunguza asili ya Acheulean katika Bonde la Olduvai, mradi wa Akiolojia wa Olduvai Gorge (OGAP) unatathmini upya mpangilio wa ki-stratigrafia, na kuchimba maeneo yenye visukuku na zana za mawe kote katika matabaka ya Olduvai.

Matabaka ya Olduvai huhifadhi vipindi muhimu vilivyodumu zaidi ya miaka milioni 2 vyenye ushahidi wa mabadiliko ya wanyama, zana za mawe na mazingira. Haya yanajumuisha kutoweka kwa Homo habilis, na kuibuka kwa Homo erectus, na mabadiliko kutoka zana za mawe za awali za Oldowan kuelekea kujitokeza kwa mwanzo kwa zana zilizoendelea zaidi za ki-Acheulean

Handaxe kutoka tovuti ya MNK

Kisukuku kutoka tovuti ya HWK EE

Malengo

Kitengo cha akiolojia kilichochimbwa huko FC East 

Kuvumbua  kisukuku huko FC West

– Uchimbuaji mkubwa katika maeneo muhimu katika Bondela Olduvai:  EF-HR, FC, MNK Fuvu,  HWK EE.

-Kufanya tafiti za majaribio katika maeoneo tofauti katika Bonde la Olduvai yanayohusiana na Oldowan na Acheulean.

– Utumiaji wa mbinu ya kuchukua sampuli ya mandhari katika matabaka ya Olduvai, kuchimba mashimo ya majaribio katika mazingira tofauti ya ikolojia ya kale.

– Uchunguzi wa kina wa stratigrafia katika maeneo, na kati ya maeneo yenye maslahi ya kiakiolojia ili kubaini uhusiano wao na muktadha wa ikolojia ya kale.

-Uundwaji upya wa mazingira ya kale ya Bonde la ziwa Olduvai lilivyokua miaka milioni mbili iliyopita.

Uchimbaji katika MNK Kuu na MNK-T5