ORACEAF Project

Kuibuka kwa Acheulean Afrika ya Mashariki (ORACEAF)- ERC Starting Grant, 2012-2016 (Grant Agreement: 283366)
Ni machache yajulikanayo kuhusu mifumo ya mabadiliko ya kibiolojia na kitamaduni itokanayo na mchakato uliosababisha kuibuka kwa Acheulean. Kidesturi, inadhaniwa kuwa mabadiliko haya makubwa ya kitamaduni yalichochewa na kuibuka kwa spishi mpya ya binadamu, Homo ergaster / erectus, na kwamba kulikuwa na mageuzi ya kiteknolojia wakati wa Oldowan ambayo hatimaye ilisababisha kuibuka kwa zana ya Acheulean. Hata hivyo, mawazo haya hayana msingi katika ushahidi wa sasa unaopatikana, lakini umejikita katika dhana ambazo zinapaswa sasa kubadilishwa.
Bonde la Olduvai (Tanzania) ni eneo ambalo Acheulean ya kwanza iligunduliwa kwa mara ya kwanza, na ambapo mtazamo wa kimapokeo wa mabadiliko ya Oldowan-Acheulean ulianzishwa. Licha ya jukumu muhimu la Olduvai kama eneo lenye mfuatano wa kumbukumbu Afrika Mashariki na kwingineko, data za awali zimepitwa na wakati na hazifai kwa majadiliano ya sasa.
Baadhi ya zana ya Oldowan kutoka HWKEE, moja ya eneo lililochimbwa na mradi wa ORACEAF
Zana ya mwanzo ya Acheulean iliyochimbuliwa kutoka eneo la EF-HR, eneo la zaidi ya miaka milioni 1.5 huko Olduvai
Kati ya 2012 na 2016, mradi wa ORACEAF ulishughulikia tatizo hili kwa kufanya utafiti wa kina Olduvai, kulingana na upatikanaji wa data mpya zilizotokana na chunguzi mpya za kimaabara na tafiti za maeneo ya kiakiolojia. Sifa ya tafiti hii kujumuisha fani mbalimbali, zilitoa mtazamo wa pamoja kwa uchambuzi wa paleoecology, akiolojia, jiolojia na geochronology ya Acheulean ya mapema huko Olduvai.
Data za ekolojia ya kale ya Olduvai iliyotokana na isotopu ya meno (Uno et al, 2018)
Kwa kutumia mtazamo wa kinadharia wa ubunifu ambao ulijumuisha maslahi katika mabadiliko ya kitamaduni, mabadiliko ya kiikolojia, na mageuzi ya kibiolojia, na mbinu za kisasa katika akiolojia, jiolojia, na taphonomy, mradi huu ulisaidia kuimarisha Olduvai Gorge kama eneo muhimu duniani la mrejeo wa kumbukumbu ya ulimwengu na uelewa wa michakato ya mageuzi ambayo ilisababisha kuibuka kwa Acheulean, utamaduni mrefu zaidi katika historia ya wanadamu.